SUMAJKT SHOES AND LEATHER PRODUCTS 

Menu

MKURUGENZI MWENDESHAJI

Kapteni Joseph Kahana Kahungi

KARIBU SUMAJKT LEATHER PRODUCTS

Kiwanda cha bidhaa za ngozi SUMAJKT Leather Products kipo eneo la Mlalakuwa, jijini Dar es Salaam na inayojishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za ngozi kwa ajili ya matumizi ya taasisi za ulinzi, shule, kampuni, pamoja na watu binafsi.

Bidhaa zinazozalishwa ni pamoja na viatu, mikanda, mabegi na mikoba.
SOMA ZAIDI

Bidhaa za Ngozi Zinazozalishwa

Buti za Kijeshi

Viatu vya Maafisa

Viatu vya Kiraia

Viatu vya Wanafunzi

Pochi za Mikanda

Mabegi

Pochi za Wanawake

Pochi

Viatu vya Wazi

Viatu vya Kazi Ngumu

Mikanda

Mikanda ya Vyeo

UBORA WA HALI YA JUU

Uzalishaji wa bidhaa za viwandani kwa sasa kwa ajili ya kufanya biashara ni mojawapo ya shughuli kuu ambazo zinaitambulisha Shirika katika tasnia ya Viwanda nchini.

Shirika hili limekuwa kichocheo katika uzalishaji, uhamasishaji, na uchangiaji wa bidhaa katika sekta ya viwanda na hivyo kushiriki moja kwa moja katika utoaji wa ajira kwa jamii ya Watanzania sambamba na kukuza uchumi wa viwanda.

HUDUMU KWA MUDA MREFU

Kiwanda hiki kilianzishwa rasmi tarehe 13 Julai 2017. Aidha, Kiwanda kilianza kwa kutumia moja ya majengo yaliyokuwa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Mlalakuwa Dar es Salaam na vyerehani vilivyokuwa vinatumiwa na Kampuni ya CAMISUMA kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za ngozi.

Kwa sasa kiwanda kimefanikiwa kununua vyerehani na mashine za kisasa za kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali.

   BAADHI WATEJA WETU   

SUMAJKT© 2022  |  Imewezeshwa na Kutengenezwa na SUMAJKT
linkedin facebook pinterest youtube rss twitter instagram facebook-blank rss-blank linkedin-blank pinterest youtube twitter instagram